IDARA YA UTABIRI WA HALI YA HEWA YAONYA KUSHUHUDIWA KWA MAFURIKO ZAIDI MWEZI HUU
Idara ya utabiri wa Hali ya Hewa nchini imetoa taarifa ikionya kwamba mvua kubwa inayonyesha katika maeneo kadhaa ya nchi itaendelea hadi mwisho wa mwezi huu, na hivyo kuongeza hatari ya mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo tofauti tofauti nchini.
Idara hiyo imeeleza kuwa mvua iliyokuwa ikinyesha mwezi Oktoba ilisababisha machafuko na iliyosababishwa na mafuriko, hasa magharibi mwa Kenya.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































