CHUO KIKUU CHA EGERTON CHAFUNGWA KWA MUDA
Wanafunzi katika chuo kikuu cha Egerton wana hadi saa nane mchana hii leo kuondoka chuoni humo kufuatia uamuzi wa baraza kuu la chama hicho kusitisha kwa muda shughuli za masomo kutokana na mgomo wa wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu.
Kupitia notisi, chuo hicho kimesema mgomo unaoendelea umeathiri pakubwa shughuli chuoni humo, na hivyo pana haja ya kusitisha shughuli hizo hadi suluhu itakapopatikana.
Hata hivyo, wanafunzi wa udaktari, sheria, wale wa kimataifa, na wale walio katika viwango vya uzamili hawataathirika na agizo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































