IEBC YAPUZILIA MBALI KUJIONDOA KWA MWANIAJI MALAVA
Utata umeibuka kuhusu mwaniaji wa chama cha DCP Edgar Busiega kujiondoa kwenye uchaguzi mdogo unaokuja eneo bunge bunge la Malava, baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kupuzilia mbali madai hayo.
Akizungumzia utayarifu wa uchaguzi huo, afisa wa IEBC anayesimamia uchaguzi huo Salim Abdalla amezitaja taarifa hizo kuwa uvumi, na kwamba mwaniaji huyo yuko debeni.
Kulingana naye, afisi yake haijapata taarifa kutoka kwa mwaniaji huyo wala chama chake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































