#Football #Sports

MERINO AIWEKA MERIKEBU YA ARSENAL KWENYE MKONDO

Mikel Merino alifunga mara 2 na kuwapa Arsenal ushindi dhidi ya Slavia Prague katika awamu ya 4 ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, na kuongeza ushindi wa mechi 10 bila kikomo kwa The Gunners katika mashindano yote.

Aidha, hii ilikuwa mechi ya 8 mfululizo ya Arsenal kutofungwa bao, wakifikia rekodi yao iliyowekwa katika misimu 2 tofauti ya mwaka wa 1903.

Merino aliwekwa kuongoza mashambulizi kwa niaba ya Viktor Gyokeres anayeuguza jeraha, na jinsi alivyofanya msimu jana katika nafasi ya Kai Havertz, hakumwagusha meneja Mikel Arteta na kutoa mchango mkubwa kwa kikosi.

Bao la kwanza la Arsenal lilikuja katika dakika ya 32 walipopewa mkwaju wa penalti ulioamuliwa kupitia VAR, na kpachikwa wavuni na Bukayo Saka kufuatia uamuzi kwamba Lukas Provod alikuwa amenawa mpira kwenye kijisanduku, kabla ya Merino kufuatisha mengine 2 katika kipindi cha pili.

Kipande kingine cha historia katika mechi hiyo ilikuwa ni ujio wa kinda Max Dowman mwenye umri wa miaka 15 na siku 308, ambaye sasa ni mchezaji mchanga zaidi kushirikishwa katika mechi ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa tangu mwaka wa 2020 na Youssoufa Moukoko alipkuwa na Borusia Dortmund.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MERINO AIWEKA MERIKEBU YA ARSENAL KWENYE MKONDO

Wabaya Bayern wamzima bingwa PSG

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *