WANASIASA, WAFUASI WAONYWA KABUCHAI
Idara ya usalama katika eneo la Bungoma Central imetoa onyo kwa viongozi wa kisiasa na wafuasi wao dhidi ya kuzua vurugu kwenye kampeni zinazoendelea ya uchaguzi mdogo katika wadi ya Chwele-Kabuchai jinsi imekuwa ikishuhudiwa.
Akizungumza baada mkutano wa kiusalama eneo hilo, kamishna wa kaunti ya Bungoma Thomas Senkei ametoa tahadhari hiyo, akisema watakaopatikana watachukuliwa hatua za kisheria.
Wakati uo huo, afisa wa tume ya IEBC eneo hilo Henry Lumiti, amehimiza kampeni za amani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































