STARS KUMENYANA NA SENEGAL MWEZI HUU
Shirikisho la soka nchini Senegal limethibitisha kwamba timu ya taifa ya Senegal maarufu kama Lions of Teranga, itamenyana na Harambee Stars ya Kenya katika mechi ya kirafiki tarehe 18 mwezi huu katika uwanja wa MArdan Sports Complex nchini Uturuki.
Mechi hiyo itaashiria kufufua kwa matumaini ya mashabiki ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona wawili hao uwanjani, baada ya mechi ya kirafiki iliyokuwa imeratibiwa kusakatwa kabla ya mashindano ya CHAN kufutiliwa mbali.
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa katika kipute cha AFCON mwaka 2019, ambako Senegal ilishinda kwa mabao 3-0 katika awamu ya makundi.
Imeatayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































