SERIKALI YATHIBITISHA MAUAJI TANZANIA
Serikali imeanzisha uchunguzi katika mauaji ya mwalimu raia wa Kenya John Ogutu aliyeuawa kwenye ghasia za baada ya uchaguzi nchini Tanzania alikokuwa akifanya kazi kama mwalimu katika eneo la Kinondoni.
Haya ni kulingana na katibu mkuu katika wizara ya usalama wa kitaifa Raymond Omollo, akithibitisha mauaji hayo kwa mara ya kwanza huku familia ya Ogutu ikilalamikia kutopewa mwanga na ubalozi wa Tanzania humu nchini.
Katika vikao vya bunge, wabunge akiwemo Babu Owino wameisuta wizara ya masuala ya kigeni kuhusiana na kuhangaishwa kwa wakenya katika mataifa ya kigeni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































