#Business

MASHARTI MAPYA YA WORLD BANK KWA MKOPO WA KENYA

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, Benki ya Dunia sasa inataka Kenya kupunguza nakisi ya bajeti yake kabla ya kupokea shilingi bilioni 96.9 kama mkopo.

Ripoti inaonyesha kuwa deni la mwaka huu wa kifedha unaoisha Juni mwaka ujao inafikia shilingi bilioni 901. Hii inaipa Hazina ya kitaifa fursa ya kupunguza matumizi au kuongeza mapato ili kupunguza upungufu.

Hali hiyo mpya ya Benki ya Dunia inaweza kuifanya serikali kuamua kuongeza ushuru na kuchukua hatua zingine za kubana matumizi.

Kulingana na benki ya dunia, Kenya bado haijakubaliana kuhusu hatua za ziada za kupunguza nakisi ya bajeti – hatua ambayo imechelewesha utoaji huo tangu tarehe iliyokubaliwa hapo awali mwezi Juni 2025.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

MASHARTI MAPYA YA WORLD BANK KWA MKOPO WA KENYA

MAGENDO YA KAHAWA SIRISIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *