MWANABLOGU MAHAMANI KWA ‘KUMCHAFULIA JINA MCA
Mwanablogu Boniface Ohindo aliyekamatwa kwa tuhuma za kumchafulia jina mwakilishi wadi wa Yimbo East eneo bunge la Bondo Francis Otiato anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii.
Afisa wa DCI eneo la Bondo Reuben Onchoka, amesema maafisa wa DCI walimkamata Ohindo baada ya mwakilishi wadi huyo kupiga ripoti akilalamikia madai ya mshukiwa kuchapisha habari potovu kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye wadi hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya Wakazi eneo hilo wametaka wawili hao kusuluhisha migogoro yao nje ya mahakama.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































