IVAN JURIC, AFUTWA KAZI
Kocha raia wa Croatia, Ivan Juric, ametimuliwa kazi na klabu ya
Atalanta baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Serie A, hali
iliyowaacha katika nusu ya chini ya jedwali
Atalanta walipokea kichapo cha mabao 3–0 nyumbani dhidi ya
Sassuolo siku ya Jumapili, matokeo yaliyowashusha hadi nafasi ya 13
kwenye msimamo wa ligi.
Klabu hiyo ya Bergamo ilikuwa imeanza msimu vizuri bila kupoteza
mechi tisa mfululizo, ingawa saba kati ya hizo ziliishia kwa sare, kabla
ya kupoteza dhidi ya Udinese na Sassuolo, matokeo yaliyosababisha
uongozi wa klabu kuchukua hatua ya kumfuta kazi Juric.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































