KESI YA MVUVI NAKURU KUENDELEA
Kesi kuhusu mauaji ya Mvuvi Brian Odhiambo aliyetoweka mapema mwaka huu katika mbuga ya wanyama ya Lake Nakuru itaendelea hii leo baada ya kurejelewa hapo jana, shahidi mmoja zaidi akiratibiwa kutoa ushahidi wake hii leo.
Kesi hiyo inawajumuisha maafisa 6 wa idara ya wanayamapori, wanaohusishwa na kutoweka kwa mvuvi huyo.
Hapo jana, mashahidi waliambia mahakama jinsi Odhiambo alichukuliwa na maafisa hao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































