KIKOSI CHA DEAFLYMPICS CHA TARAJIWA KUTOKA NCHINI HII LEO
Kikosi cha kwanza cha wanariadha na maafisa wa Kenya kinatarajiwa
kuondoka nchini hiieo kuelekea Tokyo, Japan, kwa ajili ya mashindano
ya Deaflympics ya majira ya kiangazi ya mwaka 2025, yatakayofanyika
kuanzia Novemba 15 hadi 26.
Mashindano hayo ambayo ni ya 25 tangu kuanzishwa kwake,
yatahusisha mataifa mbalimbali, huku Kenya ikishiriki katika michezo
mitano kati ya 21 itakayoshindaniwa — ikiwemo riadha, mpira wa
kikapu kwa wanawake, mpira wa mikono kwa wanaume, gofu, na
uogeleaji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa timu ya Kenya, Duncan Kuria, amesema
kundi la kwanza la wajumbe 180 litaondoka jioni ya leo, kundi la pili
kesho Jumatano, na kundi la mwisho Alhamisi.
Kenya inatarajia kuibuka na matokeo bora zaidi, kufuatia maandalizi
ya muda mrefu yaliyolenga kuinua viwango vya wanamichezo wenye
ulemavu wa kusikia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































