MAHAKAMA YATIA PINGU USAJILI WA POLISI
Vijana wanaolenga kujiunga na idara ya polisi wamepata pigo kwa mara nyingine tena baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kuzuia kwa muda zoezi la usajili lililokuwa limeratibiwa kufanya tarehe 17 mwezi huu.
Kwenye uamuzi katika kesi iliyowasilishwa na mkenya kwa jina Eliud Matindi, jaji Bahati Mwamuye ameamuru kwamba zoezi hilo lisitishwe hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Mlalamishi anahoji kuwa ni tume ya kitaifa ya huduma kwa polisi NPSC, ndiyo yenye mamlaka kikatiba kuendesha usajili huo na wala si inspekta mkuu wa polisi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































