MWONDOANO WA CAF KUCHEZWA WIKI HII
Mechi za mwondoano wa timu za shirikisho la soka barani Afrika CAF zimeratibiwa kuanza Alhamisi wiki hii, timu hizo zikiwania nafasi moja ya kumenyana na mataifa kutoka mabara mengine ili kupata nafasi ya kufuzu kombe la dunia mwaka ujao.
Mataifa ya Cameroon, Gabon, Nigeria na DR Congo yatamenyana kupata mwakilishi wa kushiriki mwondoano wa mabara yaani intercontinental playoff mwezi Machi mwaka ujao kabla ya kipute cha kombe la dunia.
Timu hizo ndizo zilimaliza katika nafasi ya pili kwa ubora katika makundi yao, na mshindi atakuwa na matumaini ya kujiunga na mataifa mengine 9 yaliyofuzu tayari kushiriki kombe la dunia nchini Marekani.
Mwondoano huo utaandaliwa katika viwanja 3 tofuati jijini Rabat nchini Morocco, Nigeria wakimenyana na Gabon huku DR Congo akikabana koo na Cameroon na kisha washindi kupamabana katika fainali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































