#Football #Sports

SOFAPAKA WACHANA BARUA ZA POSTA

Klabu ya Sofapaka ilipata ushindi muhimu wa ligi kwa kuicharaza Posta Rangers mabao 2-0 hapo jana kwenye uwanja wa Dandora jijini Nairobi.

Wachezaji Daniel Nganga na Josesph Kuloba, waliwafungia Batoto ba Mungu mabao hayo muhimu na kuwapa pointi 3 ambazo zinawaweka katika nafasi ya 7 kwa pointi 11, 5 nyuma ya vigogo Gor Mahia kwenye msimamo wa ligi kuu KPL.

Katika mechi za National Super League, Mombasa United waliendeleza msururu wa matokeo bora kwa kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Darajani Gogo.

Eric Adem aliwafungia Gogo kabla ya Neville Amwai kufunga bao la ushindi kwa wenyeji baada ya mchezaji wa Gogo kujifunga.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SOFAPAKA WACHANA BARUA ZA POSTA

WALIMU WAKUBALI KUINGIA SHA

SOFAPAKA WACHANA BARUA ZA POSTA

MWONDOANO WA CAF KUCHEZWA WIKI HII

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *