WAKENYA WAONYWA DHIDI YA SIASA UGENINI
Serikali imewaonya wakenya dhidi ya kujihusisha na siasa za mataifa mengine, ikisema mwenendo huo unaweza ukawa hatari.
Katika kikao cha kiteknolojia na vijana jijini Eldoret, Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amesema kumeshuhudiwa ongezeko la wakenya wanaojipata katika hali tatanishi, wakihitaji msaada wa serikali katika mataifa ya kigeni.
Aidha, amewatahadharisha vijana dhidi ya kuishambulia serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































