AFUENI YA RIBA KWA WAMILIKI WA ARDHI
Wamiliki wa ardhi wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Baraza la Mawaziri kuidhinisha msamaha wa riba na adhabu kwa mikopo ambayo haijalipwa ya makazi katika hatua inayolenga kuwapunguzia mzigo wa kifedha wakaazi wa kipato cha chini na kuendeleza Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi (BETA).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, uamuzi huo unafuatia mapendekezo ya Bodi ya Wadhamini ya hazina ya makazi na ardhi, ikibainika kuwa wakazi wengi wametatizika kulipa riba iliyopatikana kutokana na matatizo ya kiuchumi na uzalishaji mdogo wa kilimo.
Msamaha huo unatarajiwa kunufaisha maelfu ya wakaazi katika miradi 520 ya makazi katika kaunti 26, ikijumuisha malimbikizi ya shilingi bilioni 12.3. Baraza la Mawaziri limesema hatua hiyo ni kufuatia juhudi za serikali za kutatua dhuluma za kihistoria za ardhi, kuongeza tija ya kilimo, na kufungua thamani ya kiuchumi ya ardhi.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































