#Sports

KENYA KUWA MWENYEJI WA UBINGWA WA TAEKWONDO

Shirikisho la mchezo wa Taekwondo nchini limeratibiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya ubingwa wa Taekwondo kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 ugani Kasarani kuanzia tarehe 3-6 Disemba.

Timu ya taifa itawajumuisha wachezaji 16, wanaume 8 na wanawake 8 vile vile.

Akizungumza baada ya uzinduzi rasmi, rais wa shirikisho hilo Suleiman Sumba amesisitiza umuhimu wa Kenya kuwa mwenyeji wa ubingwa huo, ambao umevutia zaidi ya mataifa 80.

Aidha, amethibitisha kwamba maafisa wa shirikisho la Taekwondo wameitaja Kenya kuwa na miundomsingi yenye ubora wa juu ya michezo hiyo kufuatia ukaguzi.

Naye kocha mkuu Samuel Kinyanjui ameelezea imani ya kikosi chake kuibuka na ushindi.

Kikosi hicho kitaelekea Ivory Coast kwa mazoezi ya wiki 2 ili kuimarisha mbinu zao na kujinoa kabla ya mashindano hayo kuanza.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KENYA KUWA MWENYEJI WA UBINGWA WA TAEKWONDO

SERIKALI YASISITIZA UMEME UPO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *