#Business

SERIKALI KUDHIBITI UAGIZAJI WA SIMU “KUU KUU”

Serikali inapanga kupiga marufuku uingizaji wa vifaa vya kielektroniki vya zaidi ya miaka 12, vikiwemo TV, friji, simu za kisasa, kompyuta, na vifaa vingine vya nyumbani na viwandani, katika hatua ya kuzuia utupaji taka wa kielektroniki.

Rasimu ya kanuni hizo, iliyopendekezwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA), inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya sumu zinazohusishwa na saratani, magonjwa ya kupumua, na kasoro za kuzaliwa.

Mapendekezo hayo pia yanalenga kuongezeka kwa wingi wa vifaa vya kielektroniki vya mitumba akmaarufu second hand na vinavyokaribia mwisho wa maisha, ambavyo vingi huingia kwa kisingizio cha michango au bidhaa za bei nafuu zilizorekebishwa.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

SERIKALI KUDHIBITI UAGIZAJI WA SIMU “KUU KUU”

ITALIA KUKOSA KOMBE LA DUNIA KWA MARA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *