WAKENYA 3 WAZUILIWA TANZANIA, MUDAVADI
Serikali imethibitisha kwamba raia wake walinaswa katika machafuko ya uchaguzi nchini Tanzania, wakenya 3 ambao ni Samuel Kagila, Stephen Ndung’u na George Odhiambo wakiwa bado mikononi mwa polisi huku wenzao 8 wakiachiwa huru bila mashtaka.
Katika taarifa, Waziri wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi, amesema kuwa Albert Kamala na mwalimu John Ogutu waliuawa nchini humo, mwili wa Ogutu ukiwa haujulikani uliko hadi sasa.
Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wa upinzani wakitafuta hifadhi ya kisiasa humu nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































