EACC: VUNJILIA MBALI TRAFIKI FISADI
Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imependekeza kuvunjiliwa mbali kwa kitengo cha trafiki katika idara ya polisi kutokana na ufisadi ambao umefanywa kuwa desturi katika kitengo hicho.
Kwenye ripoti yake, EACC imesema ukaguzi uliofanywa kati ya Februari na Juni mwaka huu unaonyesha kitengo hicho ndicho kilichooza zaidi, waathiriwa wakubwa wakiwa wamiliki wa magari, wahudumu wa boda bod ana wasimamizi wa SACCO mbali mbali.
Mapendekezo mengine ni utekezaji kiikamilifu wa sheria ya huduma ya polisi na ukaguzi wa mara kwa mara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































