MAGAVANA WAONYA AKINA MAMA WANAJIFUNGULIA NYUMBANI
Hatua ya wizara ya afya kusitisha ufadhili kwa huduma za uzazi katika hospitali za level 2 na zahanati imewaweka hatarini akina mama wanaojifungua katika maeneo ya mashinani, idadi ya wanaojifungua hospitalini sasa ikiripotiwa kupungua.
Haya ni kwa mujibu wa magavana wakizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa Pamoja wa uangalizi wa huduma za kujifungua, wakihofia kwamba huenda akina mama hao wanajifungulia nyumbani.
Wizara ya afya ilisitisha ufadhili huo kwa misingi kwamba vituo hivyo havina vitanda vya kutosha.
Imeatayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































