NCIC: JAMII 5 ZINASHIKILIA 70% YA KAZI KATIKA MASHIRIKA YA SERIKALI
Ukaguzi mpya wa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano NCIC unaonyesha kuwa makabila matano makubwa zaidi nchini yanaendelea kutawala ajira ya umma, yakidhibiti zaidi ya asilimia 70 ya kazi katika mashirika ya Serikali.
Kulingana na ripoti hiyo, jamii za kikuyu, kalenjin, Luo, Luhya na Kamba pamoja na Kisii, Meru na Mijikenda wanachukua asilimia 88 ya nyadhifa zote katika mashirika yote ya umma. NCIC inaonya kwamba utawala huu ulioimarishwa, unaoendeshwa kwa kiasi kikubwa na upendeleo wa kisiasa, unaleta tishio kubwa kwa umoja wa kitaifa.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa jamii hizo nane zinadhibiti asilimia 86 ya kazi zote za Mkurugenzi Mtendaji, huku wanne tu kati yao wakiwa wa kutoka jamii za kikuyu, kalenjin, luo na luhya wakichukua karibu theluthi mbili ya nafasi za uongozi wa juu. Ukaguzi unaonyesha zaidi pengo kubwa la kijinsia. Asilimia 62 ya wafanyakazi wa mashirika ya Serikali ni wanaume, wakati wanawake wanashikilia asilimia 22 tu ya nyadhifa za Mkurugenzi Mtendaji, chini ya kiwango cha kikatiba cha jinsia.
Imetayarishwa na Mourine Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































