#Local News

UBINAFSI WA JAMII KUBWA WAFICHULIWA

Jamii 5 kuu nchini ambazo ni Kamba, Luhya, Kikuyu, Luo na Kalenjin zinashikilia zaidi ya asilimia 70 ya ajira katika mashirika ya umma nchini, hofu ikiibuliwa kuhusu kusambaratika kwa mshikamano wa kitaifa kutokana na mwenendo huo.

Katika ripoti ya ukaguzi, tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC imesema kwa Pamoja na jamii za Gusii, Mijikenda na Meru, jamii hizo zinashikilia asilimia 88 ya nafasi zote kwenye mashirika hayo, huku jamii 37 za watu wachache zikilazimika kugawana asilimia 12 iliyosalia.

Hospitali ya Moi imetajwa kuwa iliyokiuka sheria ya ujumuishwaji pakubwa, NCIC ikiahidi kufanya ukaguzi katika ngazi zote za serikali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UBINAFSI WA JAMII KUBWA WAFICHULIWA

RUTO ATOA HATIMILIKI 15000 KITUI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *