GAVANA WA NYAMIRA KUBANDULIWA MAMLAKANI
Mwakilishi wadi ya bonyamatuta Julius Matwere amewasilisha rasmi hoja inayolenga kumwondoa ofisini gavana wa kaunti ya Nyamira Amos Nyaribo.
Akiwasilisha hoja hiyo bungeni mapema hii leo Matwere amemtuhumu gavana Nyaribo kwa kuvunja sheria na utumizi mbaya wa mamlaka kama vyanzo vikuu vya kutaka gavana huyo atimuliwe ofisini.
Hili ni jaribio la tatu kwa wakilishi wadi wa bunge la kaunti hiyo kujaribu kumtimua mamlakani gavana Nyaribo miaka miwili baada ya majaribio mengi mawili kugonga mwamba.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































