KENYA KUJIOKOA KWENYE DEAFLYMPICS
Kikosi cha Kenya kinachoshiriki mashindano ya Deaflympics ya mwaka huu jijini Tokyo, Japan kitalenga kusaka medali yake ya kwanza hii leo, baada ya kuanza vibaya mashindano hayo kwa kichapo kufuatia kushindwa kwa timu ya handiboli ya wanawake kwenye mashindano hayo hapo jana.
Timu hiyo ya wachezaji wasio na uwezo wa kusikia ilicharazwa pointi 104-30 mikononi mwa miamba wa mchezo huo Astralia kwenye mechi ya ufunguzi.
Hata hivyo, Kenya inalenga kujikomboa hii leo kupitia fainali za mbio za mita 10,000 kwa wanaume na zile za kupokezana vijiti kwa wanawake.
Kwa upande wa wanaume, Ian Wambui atawaongoza wenzake, wengine wakiwa Peter Ruto na David Kipkogei.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































