#Football #Sports

STARS WADHALILISHWA NA SIMBA WA TARANGA

Katika tukio la aibu kwa taifa ambalo hakuna atakayetamani kulikumbuka nchini, timu ya taifa ya soka Harambee Stars ilipepetwa kama mtama na wenzao wa Senegal kwenye mechi ya kirafiki, wakibebeshwa shehena la magoli 8-0.

Mara ya mwisho kwa Kenya kudhalilishwa machoni pa ulimwengu ulikuwa mwaka wa 1978, walipocharazwa magoli 9-0 dhidi ya Zambia, historia ambayo nusra Senegal ivunje jana usiku.

Historia itakayosalia kwa kipindi kirefu ni kichapo cha mabao 13-2 dhidi ya Black Stars wa Ghana mwaka wa 1962.

Senegal wanaoorodheshwa katika nafasi ya 18 katika jedwali la FIFA ulimwenguni, waliweka kikosi kizito cha wachezaji akiwemo mshambulizi wa zamani wa Liverpool Sadio Mane aliyefunga mara 3, na Nicholas Jackson wa Chelesea ambaye yuko Bayern kwa mkopo, naye akifunga mara 2.

Haki kuelekea mapumzikoni, Simba wa Taranga, jinsi Senegal wanavyofahamika, walikuwa wamefunga mara 6, walihakikisha Stars wanahitaji Harambee ya kubeba magoli kurejea Nairobi.

Ibrahim Mbaye alifunga bao la 7 kunako dakika ya 47, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Senegal kufunga mabao mengi kiasi hicho tangu ushindi wa 7 mtungi dhidi ya Mauritius Oktoba mwaka wa 2010.

Matumaini ya pekee ya kuimarika kwa Harambee Stars yalionekana katika dakika ya 73 wakati Ovella Ochieng alijipata katika eneo la hatari na pasi kutoka kwake Sharif Musa, ila akakosa kufunga.

Hata hivyo, matumaini hayo yalizimwa kunako dakika ya 80, Pepe Cherif Ndiaye alifanya mambao kuwa 8-0 kupitia mkwaju wa penalti.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

STARS WADHALILISHWA NA SIMBA WA TARANGA

PIGO LA MAJERAHA KATIKA SAFU YA ULINZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *