#Football #Sports

HAKIMI AWAPIKU SALAH, OSIMHEN KUIBUKA BORA AFRIKA


Nahodha wa timu ya taifa ya Morocco Achraf Hakimi amechaguliwa kama mchezaji bora wa bara Afrika mwaka huu, na kutia nakshi kwenye msimu wake ambapo pia alishinda taji la klabu bingwa la bara Ulaya na klabu yake ya PSG ya Ufaransa.

Hakimi mwenye umri wa miaka 27 vile vile alishinda taji la 4 la Ligi kuu ya soka ya Ufaransa Ligue 1 msimu jana, French Super Cup na UEFA Super Cup, ila klabu yake ikalemewa na Chelsea katika kipute cha klabu bingwa ulimwenguni.

Beki huyo wa wing’i ya kulia aliwania taji hilo na washindi wawili wa awali- Mmisri Mo Salah anayewajibikia Liverpool na mshambuliaji wa Nigeria Viktor Osimhen na kushinda taji hilo la mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya kwanza.

Kwa sasa Hakimi anauguza jeraha la muundi wa mguu na iwapo atapona kwa wakati, atawaongoza Morocco katika kipute cha taifa bingwa barani Afrika AFCON mwaka huu mwezi ujao wanapowinda kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1976.

Katika kategoria ya wanawake, Ghizlane Chebbak wa Morocco ndiye mshindi wa tuzo hiyo, Wamoroko wengine wakiwa Yassine Bounou kama golikipa bora wa mwaka kwa wanaume, nayo timu ya taifa ya Morocco ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 ikichaguliwa kama timu ya wanaume ya mwaka.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cape VerdePedro Leitao Brito maarufu kama Bubista, alichaguliwa kama kocha wa mwaka baada ya kuliongoza taifa hilo kufuzu dimba la kombe la dunia litakalaondaliwa mwaka ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HAKIMI AWAPIKU SALAH, OSIMHEN KUIBUKA BORA AFRIKA

CAF YAMTUZA RUTO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *