#Football #Sports

EZE AIMARISHA MATUMAINI YA ARSENAL EPL

Kiungo wa Arsenal Eberechi Eze aliwaonyesha Tottenham Hotspurs Walichokosa walipokosa saini yake mwanzoni mwa msimu na kujiunga na Arsenal, alipofunga mabao 3 kwenye ushindi wa Arsenal wa mabao 4-1 dhidi ya Spurs kwenye debi la North London hapo jana.

Vijana wa Mikel Arteta walionyesha ubabe kuanzia kipenga cha kwanza hadi cha mwisho, bao la ufunguzi likifungwa na Mbelgiji Leandro Trossard.

Licha ya shuti la Richarlison kupunguza mwanya, lilisalia kuwafuta machozi Spurs, ushindi wa Arsenal ukiwaweka pointi 6 kileleni mwa jedwali.

Hatriki yake Eze ilikuwa ya 4 kwenye debi hiyo, baada ya nyingine 3 kufungwa na Ted Drake, Terry Dyson na Alan Sunderland.

Kwa sasa Arsenal wanajiandaa kwa pambano dhidi ya Bayern Munich kwenye kipute cha kalbu bingwa bara Ulaya Jumatano kabla ya safari kuelekea Stamford Bridge kuchuana na Chelsea wanaoshikilia nafasi ya 2.

Azma ya the Gunners kutwaa taji la EPL msimu huu baada ya zaidi ya miaka 20 lilipigwa jeki na kipigo cha washindani wake Manchester City waliopoteza 2-1 dhidi ya Newcastle, na Liverpool waliodhalilishwa nyumbani kwa mabao 3-0 na Nottingham Forest.

Manchester United watashuka dimbani dhidi ya Everton hii leo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

EZE AIMARISHA MATUMAINI YA ARSENAL EPL

JUNIOR STARS WAJIANDAA KWA S SUDAN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *