GACHAGUA, KINDIKI WAENDELEZA UBABE
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mdogo eneo bunge la Mbeere North kaunti ya Embu, serikali na upinzani umeendelea kulaumiana kuhusiana na tuhuma za kupanga vurugu siku ya uchaguzi huo, huku mirengo hiyo ikiendelea kuonyeshana ubabe wa kisiasa.
Kwa mujibu wa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, serikali imepanga kuwazuia wafuasi wa mwaniaji wa DP Newton Karish kupitia vurugu kushiriki uchaguzi, huku naibu rais Kithure Kindiki akionya upinzani dhidi ya kuzua vurugu.
Kindiki anampigia debe mwaniaji wa UDA Leo Wamuthende.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































