#Business

BENKI YA DUNIA YAPANDISHA MAKADIRIO YA UKUAJI WA UCHUMI KENYA

Benki ya Dunia imeinua makadirio ya ukuaji wa uchumi wa 2025 wa Kenya hadi asilimia 4.9, marekebisho ya juu kutoka asilimia 4.5 mwezi Mei, na kuweka historia mpya kabisa kwa nchi ya kenya.

Katika ripoti yake ya Marekebisho ya Uchumi wa Kenya mjini Nairobi, mkopeshaji huyo wa kimataifa amesema kuwa mfumuko mdogo wa bei, kurahisisha sera ya fedha, na kuimarika kwa ukuaji wa mikopo, kwa kiasi kutokana na hali ya kifedha ya makazi, vinatarajiwa kusaidia mapato ya kaya na uwekezaji wa kibinafsi.

Kulingana na benki hiyo, makadirio ya ukuaji wa uchumi wa muda wa kati unatarajiwa kusaidia ongezeko la pato halisi la kila mtu, lakini kasi ya kupunguza umaskini itasalia kuwa ndogo isipokuwa ukuaji huo utaleta mapato ya juu na kazi bora, haswa kwa masikini.

Mkopeshaji amebainisha kuwa pato la taifa kwa kila mwananchi linatarajiwa kukua kwa asilimia 2.5 mwaka 2025 na asilimia 3.0 mwaka 2026-2027, huku kiwango cha umaskini cha kimataifa kinatarajiwa kupungua kwa nusu asilimia hadi asilimia 43.2 mwaka 2026.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

BENKI YA DUNIA YAPANDISHA MAKADIRIO YA UKUAJI WA UCHUMI KENYA

MAN U WAPIGWA NA WACHEZAJI 10

BENKI YA DUNIA YAPANDISHA MAKADIRIO YA UKUAJI WA UCHUMI KENYA

KAULI YA SHOLLEI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *