#Football #Sports

GOR WALENGA KUDUMISHA UONGOZI

Mabingwa mara 21 wa ligi kuu ya Kenya KPL Gor Mahia, watalenga kuendeleza uongozi wa ligi hiyo watakapovaana na APS Bomet saa kumi alasiri hii leo.

Gor walio na mechi 2 mkononi, wanaongoza ligi kwa pointi 19, 1 mbele ya Kakamega Homeboyz na 5 mbele ya mahasimu wao wa jadi AFC leopards walio katika nafasi ya 3.

Katika mechi ya hapo jana, Ulinzi Stars waliwatandika Sofapaka magoli 3-1 na kuchupa hadi nafasi ya 9 kwa pointi 12 kutokana na mechi 10.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GOR WALENGA KUDUMISHA UONGOZI

JUNIOR STARLETS ROBO FAINALI

GOR WALENGA KUDUMISHA UONGOZI

MAN U WAPIGWA NA WACHEZAJI 10

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *