SHEREHE YA PEP YATIWA DOA ULAYA
Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola aliadhimisha mechi yake ya 100 na klabu hiyo katika dimba la klabu bingwa bara Ulaya kwa kichapo cha magoli 2-0 jibu ugani Etihad na Bayer Leverkusen.
Guardiola aliyefanya mageuzi 10 kwenye kikosi kilichopoteza mikononi mwa Newcastle Jumamosi usiku akilenga kuwapumzisha wachezaji mahari akiwemo fowadi Erling Haaland, alijipata pabaya baada ya vijana wake kupepetwa kama mtama na wageni wao.
Leverkusen walitegemea mashambulizi ya kushtukiza, na kupata ujira wao kunako dakika ya 23 kupitia kwa Alejandro Grimaldo kabla ya Patrick Schick kutia pilipili na chumvi kwenye vidonda vya City katika dakika ya 54.
Guardiola aliwaleta wachezaji wake mahiri akiwemo Haaland, Foden, Doku na Ryan Cherki katika kipindi cha 2 kwenye misheni ya uokoaji, ila juhudi zake zikaambulia patupu.
Zikiwa zimesalia mechi 3, City watahitaji kujizatiti ili kuepuka kushiriki mwondoano ilivyofanyika msimu jana.
Katika matokeo mengine, Chelsea waliwanyamazisha Barcelona kwa kichapo cha magoli 3-0 ugani Stamford Bridge, mabao yao yakifungwa na Joules Kounde aliyejifunga, Estevao Willian na Liam Delap.
Mashindano hayo yanaendelea hii leo usiku.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































