KOMBE AREJESHWA MAMLAKANI MAGARINI
Mgombeaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kwa tiketi ya ODM Harrison Kombe, ameibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika eneo hilo hapo jana.
Kulingana na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, Kombe amepata jumla ya kura 17,909, dhidi ya mshindani wake Stanley Kenga wa DCP aliyepata kura 8,907.
Kiti hicho kiliachwa wazi mapema mwaka huu baada ya mahakama kufutilia mbali ushindi wa Kombe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 kutokana na wizi wa kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































