ARTETA ATETEA ARSENAL, FODEN AKIOKOA CITY
Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa klabu hiyo inastahili heshima licha ya sare ya bao 1 dhidi ya Chelsea ugani Stamford Bridge.
Arsenal walio na orodha ya majeruhi, walijizatiti na kuokoa pointi, baada ya Chelsea waliokuwa 10 kufuatia kadi nyekundu ya kiungo Moses Caicedo kuchukua uongozi kupitia kwa Trevor Chaloba.
The Blues walilazimika kucheza dakika 61 wakiwa 10, ila wakaionyesha Arsenal kwanini ndio mabingwa wa dunia.
Arsenal walilazimisha sare kupitia kwa Mikel Merino.
Hata hivyo, Arteta ameelezea kufurahishwa na mchezo wa vijana wake, ikizingatiwa kuwa walianza bila mabeki wao muhimu William Saliba na Gabriel Magalhaes kwa mara ya kwanza msimu huu.
Katika matokeo mengine, mabao ya Phil Foden dakika ya kwanza na dakika ya 91 yaliihakikishia Manchester City ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Leeds, City sasa wakiwa pointi 5 nyuma ya viongozi Arsenal katika nafasi ya 2.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































