#Football #Sports

MATUMAINI YA NAIBOIS CAF YAFIFIA

Azma ya klabu ya Nairobi United kuingia awamu ya mwondoano katika dimba la mashirikisho ya CAF lipata pigo jingine hapo jana baada ya kupokezwa kichapo cha bao 1-0 nyumbani dhidi ya AS Maniema ya DR Congo.

Hicho kilikuwa kichapo cha pili baada ya kupoteza mechi ya ufunguzi ya makundi wikendi iliyopita dhidi ya Wydad Casablanca.

Kwa sasa Naibois ndio wa mwisho kwenye Group B ya michuano hiyo bila alama na deni la mabao 4, wakikabiliwa na hatari ya kubanduliwa nje ya mashindano hayo ambayo wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Limbukeni hao watamenyana na Azam ya Tanzania ambao pia wamepoteza mechi zao zote 2 mapema mwaka ujao, wakihitaji kupata ushindi kwenye mechi hiyo na nyingine 2 za marudiano dhidi ya Wydad na AS Maniema ili kufua matumaini ya kufuzu awamu ya mwondoano.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MATUMAINI YA NAIBOIS CAF YAFIFIA

JUNIOR STARS WAZIMWA NA TANZANIA

MATUMAINI YA NAIBOIS CAF YAFIFIA

HOMEBOYZ WAPOTEZA FURSA TENA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *