CITY KUPUNGUZA MWANYA NA ARSENAL
Manchester City wana fursa ya kupunguza mwanya wa pointi kati yao na viongozi wa ligi kuu ya Uingereza EPL Arsenal, watasafiri Craven Cottage kupambana na Fulham leo usiku.
City ambao walilazimika kusubiri hadi dakika za majeruhi kupata point izote 3 dhidi ya Leeds United, wana pointi 25, 5 nyuma ya Arsenal ambao wataialika Brentford hapo kesho.
Kwenye mechi ya City, fowadi Erling Haaland atalenga kumaliza ukame wake wa mechi 3 bila kufunga, ambao pia umemnyima fursa ya kufikisha magoli 100 kwa klabu hiyo.
Aidha, kipa Gianluigi Donnarumma anakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku mechi moja iwapo atapata kadi ya njano, akiwa tayari na njano 4.
Akizungumza na wanahabari kabla ya mechi ya leo, kocha mkuu Pep Guardiola amesema Donnarumma ana uwezo kama mtu mzima kujifunza na kujizuia dhidi ya kuendelea kupata kadi za njano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































