ICC YAFUNGA RASMI UCHUNGUZI KENYA
Hatimaye miaka ya uchunguzi kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 imefikia kikomo baada ya mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC kufunga rasmi uchunguzi wake kuhusu hali ya Kenya.
Katika taarifa yake, afisi ya mwendesha mashtaka mahakamani humo Karim Khan, imesema ilikamilisha uchunguzi wake kuhusu ghasia hizo Novemba 27 mwaka 2023.
Licha ya kufunga faili za washukiwa wakuu, ICC imesema bado inawafuatilia washukiwa 2 zaidi ambao hawajakamatwa, ikisema walihitilafiana na mashahidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































