HAKIMI AJUMUISHWA KIKOSINI MOROCCO LICHA YA JERAHA
Timu ya taifa ya soka ya Morocco imemjumuisha nahodha Achraf Hakimi katika kikosi cha wahezaji 26 wataowakilisha taifa hilo katika kipute cha taifa bingwa barani Africa AFCON kitakachoandaliwa nchini humo wiki ijayo.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 27, aliumia muundi wa mguu kwenye mechi kati ya klabu yake ya PSG na Bayern Munchen mwezi jana kwenye ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Akizungumza baada ya droo ya dimba la kombe la dunia litakaloandaliwa mwaka ujao, kocha wa Morocco Walid Regragui alisema wana matumaini Hakimi atakuwa shwari kabla ya mechi dhidi ya Comoros kwenye mechi ya ufunguzi.
Hakimi maajuzi alitawazwa kama mchezaji bora wa Afrika, na timu yake imewekwa kwenye Group A na Comoros, Mali na Zambia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































