KENYA YAPATA MEDALI ZA KWANZA ANGOLA
Kikosi cha Kenya katika michezo ya vijana kimepata medali za kwanza katika mashindano yanayoendelea nchini Angola ya 2025 African Youth Games kwa kujizolea nishani 2 za shaba katika siku ya kwanza.
Timu ya Carter ilikuwa ya kwanza kunyakua nishani yake, na kuweka msingi kwa nishani zaidi kwa taifa kwenye mashindano hayo kabla ya Margaret Nyevu kuongeza medali zaidi.
Medali hizo zimeimarisha morali ya vijana wa Kenya katika mashindano hayo yanayojumuisha michezo mbali mbali ambayo yanatumiwa kama jukwaa la kufuzu mashindano ya Youth Olympic Games mwaka huu jijini Dakar.
Kenya hata hivyo ilianza vibaya kwenye mchezo wa table tennis kwa wavulana baada ya kupoteza 3-2 dhidi ya Eritrea, nayo ya wasichana ikinyugwa na Nigeria.
Michezo hiyo itakamilika tarehe 20 mwezi huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































