#Football #Sports

KPL YAENDELEA HUKU KCB FC IKIPANDA

Ligi kuu ya soka KPL inaendelea hii leo ambapo mechi kadhaa zimeratibiwa kuchezwa katika nyuga mbali mbali.

APS Bomet watakuwa wenyeji wa Posta Rangers, Bidco United waialike Mathare United, Kakamega Homeboyz dhidi ya Shabana huku Nairobi United wakilenga kujifufua watakapokutana na Murang’a Seal.

Pambano kali litakuwa kati ya Bandari na Gor Mahia, Gor wakilenga kuondoa aibu ya kudhalilishwa a shemeji walipotitigwa bao 1-0 ya uchungu na AFC Leopards Jumapili.

Katika matokeo jana, KCB FC ilivuna ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Ulinzi Stars, na kupanda hadi nafasi ya 6 kutoka nafasi ya 8.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KPL YAENDELEA HUKU KCB FC IKIPANDA

KENYA YAPATA MEDALI ZA KWANZA ANGOLA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *