WANAFUNZI WA GREDI YA 9 KUJIUNGA NA SENIOR SCHOOL
Waziri wa elimu Julius Ogamba ametoa hakikisho kuwa watahiniwa wote milioni 1.1 wa KJSEA mwaka huu watajiunga na sekondari kuu yaani senior school ambapo watawekwa katika mojawapo ya mikondo 3 ambayo ni Sanaa na michezo, sayansi za kijamii na Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati maarufu kama STEM.
Kulingana na Ogamba, masomo kama vile sayansi jumuishi ama integrated sayansi na social studies, CRE na Kiswahili ndyio yalitia fora kwenye tathmini hiyo ya KJSEA.
Asilimia 75 ya watahiniwa iliafikia alama ya kukaribia matarajio.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































