LEOPARDS WAKATWA KUCHA INGO DERBY
AFC Leopards walipoteza nafasi kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya soka nchini KPL, baada ya kupokezwa kichapo cha bao 1-0 na Kakamega Homeboyz uwanjani Nyayo jijini Nairobi.
Licha ya kutoshana pointi wakiwa na 24, Homeboyz wanaidunisha Leopards kwa ubora wa mabao, wakirejea kileleni baada ya kupoteza nafasi hiyo mwanzoni mwa msimu.
Bao la Henry Omollo katika dakika ya 2 ya mchezo lilitosha kuwakata kucha Ingwe waliokuwa wakiongoza ligi hiyo kuelekea mapumziko ya Krisimasi.
Katika matokeo ya mechi nyingine yah apo jana, Nairobi United walipata ushindi muhimu ugenini, kwa kuipokeza Shabana FC kichapo cha mabao 3-1 ugani Gusii Stadium.
Ushindi huo unawaweka Naibois katika nafasi ya 9 kwa pointi 19, nao Shabana wakishuka hadi nafasi ya 5 kwa pointi 23, 1 nyuma ya viongozi Homeboyz na Leopards.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































