DUALE, KUCO WAKOSA MWAFAKA
Huenda wakenya wakaendelea kuhangaika kupata matibabu kutokana na mgomo wa maafisa wa kliniki unaoendelea kutokana na mvutano kati ya viongozi wa muungano wa maafisa hao KUCO na Waziri wa afya Aden Duale, ambaye amedinda kutia saini mkataba wa maelewano ya kurejea kazini ulioidhinishwa na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC.
Kwa mujibu wa Duale, mkataba huo unawahusisha maafisa wa kliniki wachache walio chini ya wizara yake, na hivyo kuwaacha nje wengi wao kote nchini, akiitaka KUCO kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya unaowajumuisha maafisa wote.
KUCO imetishia kuanzisha mchakato wa kumtimua Duale.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































