#Local News

RUTO: RIPOTI YA DHULUMA ITAZINGATIWA

Rais William Ruto ametoa hakikisho kuwa serikali itachukua hatua mwafaka kuhusu mapendekezo ya ripoti ya jopokazi la kiufundi kuhusu dhuluma za kijinsia nchini yakiwemo mauaji dhidi ya wanawake.

Akitoa hakikisho hilo, Rais amesema mapendekezo hayo yanahitaji hatua za haraka kuchukuliwa, akisema wanawake na wasichana ndio waathiriwa wakubwa wa dhuluma za kijinsia licha ya jinsia zote kuathirika.

Jopokazi hilo linaloongozwa na aliyekuwa naibu jaji mkuu Nancy Barasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *