MAHAKAMA YAWAAGIZA MADAKTARI WA KONGO, WIZARA KUELEWANA
Mahakama kuu imeziagiza pande husika katika mzozo unaowahusisha madaktari raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaohudumu nchini na wizar ya afya kutatua mgogoro huo kupitia mazungumzo, kufuatia mwasilisho wakati wa kutajwa kwa kesi hiyo.
Kesi hiyo imetajwa mbele ya jaji Roseline Aburili, ambako madaktari hao wapatao 50, wanapinga wanachokitaja kama uamuzi wa kiholela na wa kinyume na sheria wa wizara ya afya kuwapokonya leseni za kuhudumu nchini.
Madaktari hao wameitaka mahakama kufutilia mbali agizo linawazuia kupata upya leseni zao kwa mwaka huu, wakisema wamekuwa wakihudumu kwa miaka.
Imetayarishwa na Antony Nypngesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































