#Local News

SALASYA AONDOLEWA MASHTAKA BAADA YA KUTII MAHAKAMA

Mahakama ya Milimani jijini Nairobi imemwondolea kesi ya uchochezi mbunge wa Mumias East Peter Salasya baada ya mbunge huyo kutii maagizo ya mahakama yaliyomtaka afanye kampeni za kuhubiri amani kote nchini.

Akitoa uamuzi huo, hakimu Paul Mutai, ameamuru kwamba Salasya amewafikia zaidi ya watu 1,000 kwenye kampeni hizo, ikiwemo mipango ya kampeni inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Mbunge huyo alifunguliwa mashtaka ya uchochezi mwezi Mei mwaka jana, akidaiwa kutoa matamshi ya chuki kwenye mitandao ya kijamii akiwalenga watu wa jamii fulani. 

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SALASYA AONDOLEWA MASHTAKA BAADA YA KUTII MAHAKAMA

MRADI WA NYOTA WAZINDULIWA KISUMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *