JOHO AWE NAIBU WA RUTO, VIONGOZI WA PWANI
Viongozi wanaoegemea chama cha ODM kutoka ukanda wa pwani wamependekeza rais William Ruto kumteua Waziri wa madini Ali Hassan Joho kuwa mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Wakiongozwa na naibu kinara wa chama hicho na gavana wa Mombasa Alduswamad Nassir, viongozi hao wamesema kwamba Joho ana tajriba ya kutosha kuwa naibu rais.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































