COTU YAPUUZILIA MBALI PENDEKEZO LA GACHAGUA
Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Kenya COTU umetoa wito kwa serikali
kuimarisha maslahi ya wafanyakazi huku ukisema kupanda kwa gharama ya maisha
kumeendelea kuongeza mzigo kwa maelfu ya familia za wafanyikazi nchini.
Akizungumza katika kikao na wanahabari, Naibu katibu Mkuu wa muungano huo Benson
Okwaro amepuuzilia mbali pendekezo la aliyekuwa Naibu rais Rigadhi Gachagua la
kuzinduliwa kwa muungano mpya wa wafanyikazi ili kushindana na ule uliopo
unaoongozwa na Francis Atuoli akitakaja pendekezo hilo kuwa la kisiasa.
Aidha amesema kuwa ni jukumu lao la kufanya kazi na serikali iliyopo ili kuhakikisha
kuwa wafanyakazi wana mazingira bora ya ajira.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































