#Local News

LINDA MWANANCHI WAKUTANA NA MAAFISA WA DCI KUHUSU USALAMA

Viongozi wa muungano wa Linda Mwananchi wakiongozwa na Gavana wa Siaya James
Orengo pamoja na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wamekutana na
uongozi wa maafisa wa uchunguzi wa kesi za jinai DCI jijini Nairobi hii leo, kujadili masuala
ya usalama na kueka mikakati za kusitisha vurugu nchini.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wameeleza wasiwasi wao kuhusu madai ya
kuwepo kwa makundi ya wahuni yanayovuruga mikutano ya kisiasa na kuhatarisha
usalama wa wananchi pamoja na viongozi wanaohudhuria mikutano hiyo.
Hata hivyo , Wamesisitiza haja ya uchunguzi wa haraka na hatua kali za kisheria
kuchukuliwa dhidi ya wahusika huku DCI ikiwahakikishia kuwa inaendelea kufanya
uchunguzi na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ili kudhibiti matukio hayo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *